Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dereva Bodaboda atupwa Jela kwa kumbaka abiria wake

Pingu Law Dereva Bodaboda atupwa Jela kwa kumbaka abiria wake

Sat, 10 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mahakama ya Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma imemuhukumu miaka 30 jela dereva bodaboda Ruben Gerishon mkazi wa Kijiji cha Mlela na kutaifisha pikipiki yake yenye namba MC 601 DLB) baada ya kukutwa na hatia ya kumbaka abiria wake (mwanamke) mwenye umri wa miaka 24.

Inadaiwa kuwa mshitakiwa alitenda kosa hilo Septemba 7, 2023 akiwa njiani baada ya kukodiwa na abiria huyo kutoka kijiji cha Kidahwe na kumpeleka kijiji cha Mlela ambapo mshitakiwa alifikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza Septemba 11, 2023.

Akitoa hukumu hiyo hakimu wa Mahakama ya wilaya ya Uvinza, Misana Majura amesema mahakama imejiridhisha pasi na shaka ushahidi uliotolewa na upande wa mashitaka na kwamba amefungwa miaka 30 ili iwe fundisho kwa wengine.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live