Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dawasa yawakimbia wananchi kwenye mtandao ya kijamii

Tue, 2 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa amesema kuna viongozi wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (Dawasa) walijitoa kwenye makundi ya mitandao ya kijamii kutokana na malalamiko ya wananchi ya kutaka maji.

Akizungumza leo Jumanne Julai 2, 2019 kwenye hafla ya utiaji saini ya miradi mikubwa sita ya maji safi na salama kwa Jiji la Dar es Salaam na miji ya Kibaha iliyofanyika jijini Dar es Salaaa, amesema kuwa kuchelewa kwa baadhi ya miradi ya maji kunasababisha wananchi kulalamika.

“Mimi huwa nasema ukweli siku zote, Watanzania wa Dar es Salaam wamesubiri maji safi pamoja na miundombinu ya maji kwa muda mrefu, kuna baadhi ya makundi kwenye mitandao, kuna kundi moja sijui la Wazo tulikuwepo pamoja, walikuwa wanalalamika sana na ni haki yao kulalamika kwa sababu kila mtu anataka maji,” amesema Profesa Mbarawa na kuongeza

“Siku moja kulikuwa na malalamiko mpaka baadhi ya viongozi wa Dawasa wakajitoa kwenye kundi, kwa sababu watu wanahitaji maji kwa muda mrefu,” amesema

Pia, amewataka viongozi hao kukamilisha miradi mbalimbali ya maji kwa haraka ili wananchi ambao wamesubiri kwa muda mrefu waweze kupata huduma hiyo muhimu.

“Naamini sasa tumejifunza na miradi yote tunayoitekeleza itaenda kwa haraka ninaloomba Dawasa na mkandarasi tusipoteze muda tena,” amesema

Pia Soma

Profesa Mbarawa amesema miradi hiyo mikubwa iliyosainiwa leo itakayowanufaisha wakazi wa Jiji la Dar es Salaam na miji ya Kibaha itagharimu Sh114.5 bilioni.

Chanzo: mwananchi.co.tz