Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dawasa yatoa tahadhari ya upungufu wa maji Dar

98413 Pic+dawasa Dawasa yatoa tahadhari ya upungufu wa maji Dar

Mon, 9 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (Dawasa) imetoa tahadhari ya upungufu wa huduma ya maji kwa siku mbili kwa  wakazi wa  Bagamoyo na jiji la Dar es Salaam. Taarifa iliuyotolewa na ofisi ya mawasiliano ya mamlaka hiyo imesema kuwa upungufu huo utakaoanza leo Jumatatu Machi 09, 2020 unatokana na maboresho katika mtambo wa uzalishaji maji wa Ruvu Chini. “Sababu ya upungufu ni maboresho ya miundombinu katika katika mtambo wa uzalishaji maji wa Ruvu Chini” imesema sehemu ya taarifa hiyo. Taarifa hiyo imetaja maeneo yatakayoathiriwa na mateboresho hayo kuwa ni pamoja na Bagamoyo, Tegeta, Bunju, Mbezi chini, Afrikana, Tanki Bovu, Mbweni, Kawe, Goba, Makongo na Lugalo. Maeneo mengine ni; Magomeni, Mikocheni, Masaki, Sinza, Kijitonyama, Oysterbay, Mwananyamala, Kinondoni, Kariakoo, Upanga na Kisutu.

Chanzo: mwananchi.co.tz