Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dawasa yatoa tahadhari ya upungufu wa maji Dar

88858 Pic+dawasa.png Dawasa yatoa tahadhari ya upungufu wa maji Dar

Tue, 17 Dec 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (Dawasa) nchini Tanzania imetoa tahadhari ya upungufu wa huduma ya maji kwa siku mbili kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam wanaohudumiwa na mtambo wa kuzalisha maji wa Ruvu Chini.

Taarifa iliyotolewa na ofisi ya mawasiliano ya mamlaka hiyo imesema upungufu huo utakaoanza leo Jumanne Desemba 17, 2019 hadi kesho Jumatano unatokana na matengenezo ya dharura katika Mtambo wa Uzalishaji Maji wa Ruvu Chini uliopo Bagamoyo mkoani Pwani.

“Kutakuwa na upungufu wa huduma ya maji kuanzia siku ya Jumanne Desemba 17, 2019  hadi siku ya Jumatano Desemba 18, 2019  kutokana na matengenezo ya dharura katika Mtambo wa Uzalishaji Maji wa Ruvu Chini uliopo Bagamoyo” imesema taarifa hiyo

Taarifa hiyo imetaja maeneo yatakayoathiriwa na matengenezo hayo huwa ni pamoja na Mji wa Bagamoyo, Vijiji vya Zinga, Kerege, Mapinga, Bunju Boko, Kawe, Kinondoni, Ilala, Temeke na Tabata.

Maeneo mengine ni; Tegeta, Kunduchi, Salasala, Jangwani, Mbezi Beach, Mlalakuwa, Mwenge, Mikocheni, Msasani Sinza,Kijitonyama, Oysterbay, Magomeni Upanga, Kariakoo,City Centre, Ilala, Ubungo Maziwa, Kigogo, Mburahati na Hospitali ya Taifa ya Muihimbili.

“Dawasa inawakumbusha wananchi kutunza na kutumia maji kwa uangalifu katika kipindi hiki cha matengenezo” imesema taarifa hiyo.

Chanzo: mwananchi.co.tz