Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dawasa yatoa taarifa njema kuhusu maji

A4ce778e81dd0c084f766b27de70a4ad Dawasa yatoa taarifa njema kuhusu maji

Sun, 6 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam(DAWASA) imesema ukosefu wa maji uliyoyakumba baadhi ya maeneo ya jiji la Dar es salaam umetokana na marekebisho yanayoendelea kufanywa katika pampu zake tatu ambazo ndani ya saa 24 hadi 36 zijazo yataweza kurejesha maji katika msukumo wake wa kawaida.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano cha Mamlaka hiyo, hadi sasa kazi ya marekebisho ya pampu moja yakiwa katika hatua za mwisho za marekebisho huku pampu mbili zikiendelea kufanya kazi.

Aidha taarifa hiyo imesema kuwa kufuatia matengenezo hayo kumesababisha huduma ya maji kuwa na upungufu wa maji wa asilimia 20 ambapo imewaomba radhi watu wote walioathirika na hali hiyo.

Imeyataja maeneo yaliyoathirika kuwa ni pamoja na Mlandizi mjini, Ruvu Darajani, Vikuruti, Disunyara na Kilangala.

Maeneo mengine iliyoyataja ni pamoja na Janga, Mbagala, Visiga, Maili 35, Zogowale, Misuvusugu, Tanita, Kobondeni, Kwa Mathiasi, Nyumbu, Msangani, Kwa Mbonde na Picha ya Ndege.

Pamoja na hayo maeneo mengine ni Sofu, Lulanzi, Gogoni, Kibamba, Njia Panda shule, Kibwegere, Mloganzilaz Kwembe, Kibamba Hospitali na kwa Mtinga. Dawasa imeyataja maeneo mengine kuwa ni luguruni, Mbezi, Kimara,Ubungo, Makongo, Tabata, Bonyokwa, Kinyerezi, Kisukuru, Kipawa na Kiwalani

Chanzo: habarileo.co.tz