Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dawasa yatangaza upungufu wa maji maeneo haya

75d6cadff92306e6aa1dec55a38d43e8 Dawasa yatangaza upungufu wa maji maeneo haya

Sat, 27 Mar 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MAMLAKA ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (DAWASA) imetangaZa saa 12 za upungufu wa huduma ya maji kwa wananchi wanaohudumiwa na mtambo wa Ruvu Juu.

Taarifa iliyotolewa na Kitengo cha Mawasiliano na Jamii cha mamlaka hiyo imesema, upungufu huo utatokea kwa saa 12 za leo Jumamosi tarehe 27 Machi 2021.

Sababu ya ukosefu wa majisafi ni kuruhusu, Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) kuboresha laini ya umeme kutoka Chalinze.

Imeyataja maeneo yatakayoathirika ni Mlandizi, Ruvu Darajani, Vikurutu, Visiga, Misugusugu, Kongowe, Soga, Maili 35, Kwa Mfipa, Mwendapole, Kwa Mathias, Mkuza, Picha ya Ndege na Shirika la Elimu Kibaha.

Mengine ni, Pangani, Maili Moja, Kibaha, Kiluvya, Kibamba, Mbezi, Temboni, Kwa Msuguri, Saranga, Golani, Stop Over, Bonyokwa na Changanyikeni.

Pia, maeneo ya Buguruni, Ubungo, Kisiwani, Msewe, Kilungule, Tabata, Segerea, Kinyerezi, Kiwalani na Pepsi mpaka Airport.

“Upatikanaji wa huduma ya maji utarejea katika hali yake ya kawaida mara tu hali ya umeme itakapotengamaa,” imeeleza Dawasa huku ikiomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza.

Chanzo: www.habarileo.co.tz