Dar es Salaam. Ofisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasa), Cyprian Luhemeja amesema ili kukabiliana na changamoto ya ukosekanaji wa maji katika baadhi ya maeneo mamlaka hiyo imeamua kutumia asimilia 35 ya mapato ya makusanyo yake ili kuendesha miradi katika maeneo mbalimbali.
Hayo ameyasema leo Jumatatu Juni 4, 2019 wakati akiwasilisha taarifa ya utendaji wa katika kipindi cha miaka mitatu cha mamlaka hiyo mbele ya wajumbe wa kamati ya siasa mkoa wa Dar es Salaam.
Akizungumza katika mkutano huo, Luhemeja amesema ili kufanikisha suala hilo walilazimika kutenga Sh4 bilioni kila mwezi inayotokana na mapato yao.
“Hii imeshapitishwa na lazima suala hilo lifanyike kila mwezi, na tumefungua akaunti maalumu benki ambayo haiguswi na kila wakati huangaliwa kama kuna kiasi kisichopunguzwa,” amesema Luhemega
Amesema kupitia fedha hizo miradi 16 katika maeneo mbalimbali inatekelezwa huku sita kati yake ikiwa imekamilika, miwili inajengwa na mingine ikiwa katika hatua mbalimbali za manunuzi ya mkandarasi.
“Tutaendelea kuhakikisha fedha hizi zinasaidia katika kuendesha miradi tunayotaka kuitekeleza badala ya kusubiri fedha kutoka kwa wahisani na serikali,” amesema Luhemega
Pia Soma
- Uturuki yakomalia dili la makombora ya Urusi
- MAUAJI YA MWANAFUNZI WA SCOLASTICA :Tafrani yaibuka hukumu mauaji ya mwanafunzi wa Scolastica
- Makonda abaini upigaji vitambulisho vya machinga Kariakoo
- Juma Nature aelezea ajali iliyotokea msafara wa Nandy Festival
Naye Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Kate Kamba alipongeza uamuzi uliochukuliwa na bodi ya Dawasa huku akibainisha ni suala la kubunia jinsi ya kutekeleza miradi kwa fedha za makusanyo linapaswa kuigwa na watu wengine.
“Unapotembeza bakuli kuomba msaada hauna uhakika lakini unapobana kidogokidogo cha kwako unakuwa na uhakika wa kufanya unachokusudia,” amesmea Kate.