Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dawasa kusaini miradi mikubwa ya kimkakati kesho

Tue, 2 Jul 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mamlaka ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam (Dawasa), kesho Jumanne Julai 2, 2019 itasaini miradi sita ya kimkakati yenye lengo la kuboresha upatikanaji kwa wakazi wa Dar es Salaam na Pwani.

Taarifa iliyotolewa leo Jumatatu Julai 1, 2019 na kitengo cha mawasiliano cha Dawasa imesema mgeni rasmi atakuwa Waziri wa Maji, Profesa Makame Mbarawa ambaye atashuhudia utiaji saini miradi hiyo yenye thamani ya zaidi ya Sh150 bilioni.

Dawasa imewaomba wananchi wakiongozwa wenyeviti wa serikali za mitaa kujitokeza kwa wingi kushuhudia shughuli hiyo itakayofanyika ofisi za Dawasa, Gerezani jijini Dar es Salaam.

Maeneo yatakayonufaika na miradi hiyo ni; Pugu, GongolaMboto,Ukonga, Majohe, Chanika, Changanyikeni, Makongo, Jeti, Mbezi Beach, Wazo, Bunju A, Salasala, Mpiji, Mwabwepancle, Goba, Kitunda, Mwanagati, Kigamboni, Chalinze na Mboga.

Miradi hiyo ambayo itakayosainiwa ni wa usambazaji maji kutoka Makongo hadi Bagamoyo; Mradi wa bomba la kusafirisha maji kutoka Jeti hadi Buza; mradi wa kuendeleza visima vya Kimbiji na mradi wa usambazaji maji Kisarawe hadi Pugu (Gongolamboto, Pugu station, Airwing, Ukonga na Majohe).

Mingine ni; Mradi wa usambazaji maji katika mji wa Mkuranga na mwisho mradi wa bomba la kusafirisha maji kutoka Mlandizi- Chalinze hadi Mboga

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz