Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dawasa kufunga bwawa la majitaka Vingunguti kwa siku 30

99742 Pic+dawasa Dawasa kufunga bwawa la majitaka Vingunguti kwa siku 30

Fri, 20 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dar es Salaam (Dawasa) nchini Tanzania limesema litafunga bwawa la majitaka vingunguti kwa muda wa siku 30 kuanzia Jumatatu Machi 23, 2020 hadi Aprili 24, 2020.

Taarifa ya Ofisi ya Mawasiliano ya Dawasa iliyotolewa leo Ijumaa Machi 20, 2020 imesema sababu za kufunga bwawa hilo ni kuruhusu ukarabati wa bwawa la kwanza eneo la kupokea majitaka kwa magari.

Dawasa imewataka waendesha magari ya kunyonya majitaka, huduma ya umwagaji majitaka itaendelea katika mabwawa ya Kurasini maarufu kama Shimo la Udongo yaliyopo Wilaya ya Temeke jijini humo.

“Tunaomba radhi kwa usumbufu wowote utakaojitokeza,” imeeleza taarifa hiyo

Chanzo: mwananchi.co.tz