Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dawa ya mganga kusafisha nyota yaua mtoto

6164365093c243c25d4ca6ddec1f173b Dawa ya mganga kusafisha nyota yaua mtoto

Tue, 19 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MTOTO Juma Megejuwa (12) mkazi wa Kijiji cha Mwaningi katika Kata ya Bulige wilayani Kahama mkoani Shinyanga, amefariki dunia baada ya kunywa dawa ya kienyeji kwa mzazi wake ambaye ni mganga wa kienyeji kwa lengo la kusafishwa nyota.

Aidha, watu wawili ambao ni ndugu, Loya Ngusa (66) na Bahati Ngusa (25) nao baada ya kunywa dawa hiyo, walizirai na kukimbizwa katika kituo cha afya kupatiwa matibabu.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Shinyanga, Debora Magiligimba, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo nyumbani kwa mganga huyo aliyefahamika kwa jina la Dela Megejuwa (44).

Magiligimba alisema mtoto huyo alifariki dunia juzi saa tisa alasiri, na kwamba, wateja wengine wawili wa mganga huyo waliokwenda kutibiwa ili kusafisha nyota akiwemo jirani wa mganga huyo na mwingine mkazi wa Shilima, Kwimba mkoani Mwanza, walizirai.

"Wateja hao wawili nao walizirai baada ya kunywa dawa (mitishamba) idhaniwayo ni sumu na kukimbizwa katika Kituo cha Afya cha Chela. Hali zao zinaendelea vizuri," alisema.

Aidha, Kamanda Magiligimba alisema baada ya tukio hilo, mganga huyo wa kienyeji alikimbia na Jeshi la Polisi linaendelea kumsaka.

Alisema mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Kahama kwa uchunguzi zaidi.

Alitoa mwito kwa waganga wa jadikuwa na uhakika wa matumizi ya dawa za kienyeji na matumizi mazuri ya vibali au leseni zao ili kuepuka vifo na madhara mengine kwa wateja wao.

Alisema Jeshi la Polisi halitamuonea huruma mganga yeyote anayekwenda kinyume na maelekezo ya vibali au leseni.

Chanzo: habarileo.co.tz