Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dawa ya Mbu yalipua magari matatu Tabata

TABATA MOTO Ajali ya Moto

Mon, 9 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Usiku wa kuamkia leo kumezuka moto katika maegesho ya magari yaliyopo maeneo ya Tabata, jijini Dar es Salaam uliodumu kwa takribani saa moja hadi pale ulipo dhibitiwa.

Ajali hiyo inatajwa kuhusuhwa na mtu kuchoma dawa ya mbu ndani ya gari ambapo moto ulilipuka na kuunguza magari takribani matatu yaliyokuw ana mizigo ndani yake. Afisa ulinzi kutoka kapuni ya ulinzi ya SGA alithibitisha kutokea kwa janga hilo, na walipo pewa taarifa walifika mara moja kuudhibiti.

"Niliwauliza chanzo cha moto ni nini wakasema sisis hatujui, ila kuna tetesi tetesi kuwa kuna mtu aliwasha dawa ya mbu ndani ya gari, na hii gari ya kati kati ndio ilianza kuwaka zikashika hizi nyingine mbili, kwahiyo gari tatu zimeungua pamoja na banda hilo la pembeni, hakuna mtu alikuwa ndani ya gari, tuliweza kuthibiti mizigo tukaitoa".

Hivi karibuni kumetokea matukio ya moto sehemu mbali mbali nchini, hali ambayo inazua minongono mingi kwa wananchI, ambao wanatoa mapendekezo kwa Mamlaka husika kuweka miundo mbinu rafiki itakayoweza kudhibiti majanga ya moto yanapojitokeza.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live