Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dau nono latangazwa utunzaji wa vyanzo vya maji

Mon, 3 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam.  Kiwanda cha mabati cha Alaf kupitia kampeni yake mpya kimetangaza dau nono kwa mshindi wa picha bora itakayoelezea umuhimu na utunzaji wa vyanzo vya maji Tanzania.

Katika kampeni iliyozinduliwa leo Jumatatu Juni 3, 2019 inayofahamika kwa lugha ya kiingereza ‘Eye in the Wild’ washiriki watatakiwa kutuma picha iliyobeba ujumbe kuendana na maudhui ya utunzaji vyanzo vya maji.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo mkurugenzi mkuu wa kiwanda hicho, Dipti Mohanty amesema lengo hasa la kampeni hiyo ni kuanzisha mjadala wa kimazingira kuhusu umuhimu wa utunzaji vyanzo vya maji.

Alaf wamezindua kampeni hiyo chini ya kampuni yake mama ya Salaf yenye matawi yake nchini Kenya, Uganda na Rwanda.

“Kwa Tanzania ni mara ya kwanza, lakini wenzetu Kenya walishafanya miaka iliyopita kwenye dhima za utunzaji mazingira na ilileta mafanikio makubwa katika kuhamasisha wananchi na wadau mbalimbali kwenye shughuli za kimazingira,” amesema.

Mahonty amesema washiriki watatakiwa kutuma picha zao kupitia tovuti ya kampuni hiyo na atakayefanikiwa kua mshindi wa kwanza kwenye shindano ataondoka na kitita cha zaidi ya dola za kimarekani 3, 000 ambacho ni zaidi ya Sh6.8 milioni.

Pia Soma

“Mshindi wa pili atapata zawadi ya dola za kimarekani 2, 000 (Zaidi ya Sh4.5 milioni) na watatu atapata dola 1, 000 (sawa na Sh2.2 milioni,” ameongeza .

Mkurugenzi huyo amesema shindano hilo litahusisha wafanyakazi wa kiwanda cha Alaf ambao watatakiwa kusambaziana picha zao na mshindi atapewa zawadi ya kamera ya kisasa zaidi aina ya Canon.

Mkuu wa kitengo cha masoko katika kiwanda hicho Isamba Kasaka amesema kupitia kampeni hiyo Alaf inalenga kuwa chachu ya uhamasishaji katika utunzaji wa mazingira Tanzania na inafanya hivyo kwa kushirikisha wadau mbalimbali kwenye sekta ya maji na mazingira pamoja na wananchi.

“Tulichagua dhima hii kwa sababu katika maeneo mbalimbali Tanzania kuna upungufu wa rasilimali ya maji na sehemu nyingine hakuna kabisa. Hii inatokana na uharibifu mkubwa uliofanyika na unaoendelea kufanyika katika vyanzo vya maji,” amesema.

“Zaidi tunataka picha ambayo ina stori  yaani iliyobeba jumbe za utunzaji wa vyanzo vya maji. Tunahamasisha watu wote kushiriki na hamasa hii ifike kote nchini,” amesema

Kasaka amesema kupitia kampeni hiyo wanategemea kupokea washiriki wengi zaidi kutokana na unyeti wa sekta yenyewe kwenye maisha ya wanadamu.

Chanzo: mwananchi.co.tz