Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Darasa walilohamishiwa kulala wanafunzi lateketea moto

Bweni Pic Darasa walilohamishiwa kulala wanafunzi lateketea moto

Wed, 15 Feb 2023 Chanzo: mwanachidigital

Siku moja baada ya bweni la wasichana Shule ya Sekondari Tamabu kuungua moto na wanafunzi kuhamishiwa darasani kwa ajili ya kulala, darasa hilo nalo limeungua moto.

Mkuu wa Shule ya Sekondari Tamabu, Lucas Barabara amesema wakati darasa hilo linaungua moto hakukuwa na umeme shuleni hapo.

Tuko hilo limetokea leo Februari 15 mwaka huu saa tisa alasili wakati wanafunzi wakiwa nje.

Jeshi la Zimamoto na Uokoajia limefika kwa wakati na kufanikiwa kudhibiti moto huo.

Hakuna mwanafunzi yoyote aliyepata madhara kutokana na tukio hilo na baadhi ya mali za wanafunzi zimeokolewa.

Chanzo: mwanachidigital