Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Daraja linalounganisha Kata tatu Bukoba lafikia asilimia 95 kukamilika

Katoro ED.jpeg Daraja linalounganisha Kata tatu Bukoba lafikia asilimia 95 kukamilika

Mon, 25 Oct 2021 Chanzo: ippmedia.com

Ujenzi wa daraja lenye kuunganisha mawasiliano kati ya kata ya Katoro, Kashaba na Kyamlaile zilizopo Wilayani Bukoba mkoani Kagera limefikia asilimia 95 ili likamilike.

Daraja hilo lililokuwa limezingirwa na maji kwa kipindi cha miaka mitatu na kusababisha Wananchi wa kata hizo kutumia mitumbwi kuvuka eneo hilo lenye umbali wa kilomita moja.

Akizungumzia ujenzi huo Mratibu wa Wakala wa Barabara Mjini na Vijiji (TARURA) Mkoa wa Kagera Avit Theodory, amesema mwaka 2018 hadi 2019 eneo hilo lilitengewa fedha kiasi cha shilingi milioni 519 kwa ajili ya ujenzi wa daraja jipya.

Aidha, amesema katika kufanikisha ujenzi wa daraja hilo jipya, wamejenga ukuta wenye mita 300, karavati 12, kujaza mawe na kuinua tuta lenye umbali wa kilomita moja ili kuruhusu maji kupita.

Chanzo: ippmedia.com