Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Daraja la Kunduchi laanza kutumika leo

Rain Pic Daraja la Kunduchi laanza kutumika leo

Mon, 22 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Daraja la Kunduchi Mtongani Jijini la Dar es salaam limeanza kupitika leo baada ya juhudi za Serikali kufanya kazi usiku na mchana kurudisha mawasiliano katika eneo hilo.

Mawasiliano darajani hapo yalikatika kutokana na kipande cha barabara kinachounganika na daraja kukatika kutokana na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia juzi maeneo mbalimbali ya Dar es salaam.

Wakazi wa Mbweni, Ununio, Bahari Beach na maeneo ya jirani sasa wameanza kupita darajani hapo baada ya awali kulazimika kutumia barabara ya uelekeo wa Tegeta Nyuki na njia nyingine mbadala.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live