Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Daraja la Dumila lapata ufa, polisi wazuia magari kulitumia

36885 Pic+dumila Daraja la Dumila lapata ufa, polisi wazuia magari kulitumia

Thu, 17 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Daraja la Dumila maarufu kama daraja la Magufuli halipitiki baada ya kujaa maji na kingo zake kuweka nyufa kutokana na mvua kubwa inayonyesha. Kujaa maji kwa daraja Hilo kunatokana na mvua iliyonyesha usiku hasa maeneo ya milimani katika wilaya za Kilosa, Mvomero na mikoa ya jirani ya Tanga na Manyara. Kutokana na kujaa maji kwa daraja hilo, magari yanayotumia barabara ya Dodoma - Morogoro yamesimamishwa kufanya safari na kutakiwa kutumia barabara ya vumbi ambayo ni mbadala ya Mkata. Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Wilbroad Mutafungwa akizungumza na MCL Digital leo Januari 16, 2019 amesema kwa sasa kinachofanyika ni kuyataka magari yote yanayotumia barabara hiyo kutumia njia mbadala mpaka hapo utaratibu mwingine utakapofanyika. "Tumesitisha magari kupita hapo darajani maana limejaa maji na kingo kuweka ufa,"amesema Mutafungwa Taarifa zaidi zitawajia punde

Chanzo: mwananchi.co.tz