Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Amos Makalla leo (Novemba) amefanya kikao kazi Cha maandalizi ya maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika ambapo amewaelekeza viongozi wa ngazi ya Mkoa, Wilaya Kata na Mitaa kulibeba Jambo hilo.
RC Makalla amesema Maandalizi ya tukio Hilo la kihistoria yanakwenda vizuri na kutoa wito kwa Wananchi kujitokeza kwa wingi siku hiyo na kueleza kuwa mkoa umejipanga kuhakikisha hali ya ulinzi na usalama inaimarishwa.
Aidha, RC Makalla amesema katika kuelekea maadhimisho hayo kutakuwa na matukio mbalimbali ikiwemo ziara za viongozi kuzindua miradi mbalimbali ya maendeleo.
RC Makalla amesema tukio hilo litahudhuriwa na viongozi wa mataifa mbalimbali wanaokuja kumuunga mkono Rais Samia Suluhu.