Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dar wapanga mkakati biashara zifanyike saa 24

35397 Pic+makonda Dar wapanga mkakati biashara zifanyike saa 24

Wed, 9 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema kabla ya Februari, 2019, ofisi yake itaruhusu rasmi wafanyabiashara kufanya shughuli zao saa 24 wakiwemo wamiliki wa baa.

Makonda ameyasema hayo leo Februari 8 wakati akizungumza na vyombo vya habari ofisini kwake.

Amesema ofisi yake ipo katika mchakato wa kukutana na wafanyabiashara kwa ajili ya kuzungumzia suala hilo na kuangalia njia zipi za kuzingatia ili kuhakikisha kunakuwa na usalama wa kutosha.

“Kabla hatujawaruhusu wafanyabiashara hawa kufanya kazi zao saa 24, kuna mengi ya kuyaandaa hasa kuhakikisha wamiliki wanajiandaa lakini pia tunafunga taa za usalama na kamera, ili kuzuia uhalifu,” amesema.

Katika hatua nyingine Makonda amesema viongozi wa jiji wapo katika maandalizi ya mwisho ya ujenzi wa ufukwe wa Coco utakaogharimu kiasi cha Sh11.9 bilioni fedha ambazo tayari zimetengwa kwa ajili ya ujenzi huo.

Amesema Coco Beach ni ufukwe ambao utaweza kutumiwa na watu wote na kutakuwa na sehemu tofauti kulingana na mahitaji ya watumiaji na hadhi zao.

“Coco Beach itajengwa kwa ajili ya makundi matatu kuanzia kwa watu wa kipato cha chini, kati na wale wa kipato cha juu,” amesema Makonda.



Chanzo: mwananchi.co.tz