Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dar kinara matumizi ya choo

Pic Choo Dar kinara matumizi ya choo

Wed, 22 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

DAR ES SALAAM imetajwa kuwa kinara wa matumizi ya choo bora nchini ikifuatiwa na Ruvuma na Njombe.

Ongezeko hilo la watu wanao tumia vyoo bora limeongezeka kutoka asilimia 21 mwaka 2016 hadi asilimia 74.8 mwaka 2022 ambapo ni hatua chanya ya kufikia lengo la 6.2 la Malengo ya Maendeleo Endelevu ya Dunia ya 2030 “Sustainable Development Goals”.

Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa za hali ya matumizi ya vyoo bora nchini Dar es Salaam inaongoza kwa asilimia 98.5, Ruvuma 92.1 na Njombe 87.6.

Kufuatia hali hiyo, Taasisi ya Utu na Mazingira (HUDEFO) imesema choo ni afya, kinalinda hadhi ya ubinadamu na utu, ni muhimu katika kuhifadhi na kulinda mazingira.

“Chooni ni sehemu ya kujistiri na kumaliza haja zilizokupeleka kama huna choo inamanisha unaenda vichochoroni, unaenda sehemu za kujificha na hapo huwi huru kama ukiwa chooni, takwimu zinaonyesha bado kuna tatizo kubwa la matumizi ya choo maana idadi kubwa ya watu hawana vyoo,”amesema na kuongeza

“Kujisaidia vichakani au kwenye vyanzo vya maji unasababisha maji yasiwe salama tena kwa watumiaji, na pia unanafasi kubwa ya kusababisha magonjwa ya mlipuko,”amesema.

Aidha, amesema elimu iendelee kutolewa kwa wananchi ili waelewe umuhimu wa vyoo na matumizi yake.

“Tunahitaji kuongea na viongozi wa jadi kuhusu mila mbali mbali nilifaya kazi Kilwa wengi wanaenda kujisaidia baharini kwa ajili ya mila zao, tukiwaelimisha itasaidia, umuhimu wa vyoo na madhara kujisaidia hovyo,sio kitu cha kufumbia macho, kama tunaweza kufanya jambo wakati ni sasa ili kukatisha desturi za watu kujisaidia hovyo vichakani na baharini, kuwe na ufuatiliaji wa sheria,”amesema. -

Chanzo: www.tanzaniaweb.live