Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dar es Salaam kuna upungufu wa madarasa 381 ya kidato cha kwanza

92584 Pic+uteuzi Dar es Salaam kuna upungufu wa madarasa 381 ya kidato cha kwanza

Wed, 22 Jan 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Imeelezwa kuwa Mkoa wa Dar es Salaam una upungufu wa vyumba vya madarasa 381 kwa ajili ya wanafunzi wanaopaswa kujiunga na kidato cha kwanza mwaka 2020.

Hayo yameelezwa leo Jumanne Januari 21, 2020 na mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda wakati akipokea msaada wa ndoo 500 za rangi wa kiwanda cha rangi cha Billioni Paint kwa ajili ya ujenzi wa vyumba hivyo vya madarasa unaoendelea maeneo mbalimbali mkoani humo.

Makonda amesema licha ya Mkoa huo kuongoza katika ufaulu katika matokeo ya mtihani wa kuhitimu elimu ya msingi mwaka 2019, wilaya ya Temeke wanafunzi 5970 wakikosa nafasi kujiunga na  kidato cha kwanza kutokana na uhaba wa madarasa. Wilaya hiyo pekee ilikuwa na upungufu wa madarasa 120.

"Kutokana na tatizo hilo Mkoa uliona katika kulishughulikia suala hilo ni vema tukajumuisha Mkoa mzima ili kutekeleza maelekezo ya Wizara ya Elimu ya darasa moja wanafunzi 50.”

Makonda amesema wapo wanaoendelea na ujenzi wa shule mpya, madarasa mapya, matundu ya vyoo na kutengeneza madawati ili kukamilisha kwa pamoja.

“Hizi rangi si ndogo, katika ujenzi huu zitatusaidia kupiga hatua na tunawahakikishia katika shule ambapo rangi hizi zitafika, darasa moja tutachora jina la kiwanda ili wanafunzi wajue kuna watu waliwachangia,” amesema.

Pia Soma

Advertisement

Chanzo: mwananchi.co.tz