Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dar: Jambazi Auawa Akipora Simu

Kingai?fit=800%2C533&ssl=1 Dar: Jambazi Auawa Akipora Simu

Tue, 20 Jul 2021 Chanzo: globalpublishers.co.tz

Dar: Jambazi Auawa Akipora Simu July 20, 2021 by Global Publishers



JESHI la Polisi Mkoa wa Kinondoni limemuua mtu mmoja anaedaiwa kuwa ni jambazi baada ya kumpora simu mama aliyekuwa akitembea kwa miguu.

Kamanda wa Polisi, Ramadhan Kingai amesema tukio hilo limetokea Jumatatu Julai 19, 2021 saa tatu kasoro wakati watu hao wakiwa na pikipiki eneo eneo la Kinondoni jirani na Dar Free Market.

Amesema baada ya tukio hilo watuhumiwa hao walianza kukimbia huku wakifyatua risasi bila kujua kama eneo hilo kulikuwa na askari jirani.

“Walikuwa watu wawili kwenye pikipiki aina ya boxer baada ya kupora simu, walianza kukimbia huku wakifyatua risasi ovyo askari wetu waliwakimbiza na kufanikiwa kumpiga risasi mmoja wao ambaye alidondoka chini,” amesema Kamanda Kingai.

Amesema katika tukio hilo walifanikiwa kupata pikipiki ania ya boxer yenye namba pamoja na bastola aina ya brown ambayo usajili wake bado haujapatikana.

“Pamoja na kuipata pikipiki tumeafanikiwa kupata simu mmoja iliyokuwa ikitumiwa na wahalifu, simu iliyoibwa pamoja na mtuhumiwa mmoja tunaendelea kumtafuta,”amesema.

Share this:TweetWhatsApp Related

Chanzo: globalpublishers.co.tz