Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dar, Dom mbioni kuwa na Kampasi ya Michezo

Fe2f38e8727d0811e688699dec54c3bf Dar, Dom mbioni kuwa na Kampasi ya Michezo

Wed, 5 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KATIBU Mkuu Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dk. Hassan Abbasi amesema dhima ya serikali ni kuanzisha Kampasi ya Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya katika Mkoa wa Dodoma na Dar es Salaam kwa lengo la kutoa fursa kwa vijana wengi kujifunza maswala ya michezo.

Dk. Abbasi ameyasema hayo leo jijini Dodoama akizungumzia mafanikio ya serikali ya awamu ya tano, na kwamba tayari uongozi wa Bodi ya Chuo hicho umekwisha pitisha azimio hilo la kuanzishwa kwa kampasi hizo mbili.

“Serikali imeendelea kuimarisha Miundombinu ya Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya kilichopo Mwanza, fedha za maendeleo zimekuwa zikitolewa kuimarisha miundombinu na kwa mwaka wa fedha ulionza Julai 2020 chuo kimetengewa fedha kwa ajili ya kuongeza Hosteli, Madarasa, na viwanja vya mazoezi kwa wanafunzi,”amesema Dk.Abbasi.

Amesema serikali imeweka mifumo ambayo inasimamia sekta ya michezo vyema ikiwemo Bazara la Michezo Taifa (BMT) kwa kushirikiana na mashirikisho mbalimbali, na katika serikali ya awamu ya tano sekta hiyo imefanikiwa kuongeza hamasa kwa wananchi kushiriki michezo kwa lengo la kuimarisha afya zao.

Sharia ya Habari:

Kwa upande wa Sekta ya Habari Dk. Abbasi alifafanua kuhusu Sheria ya Huduma za Habari ya Mwaka 2016 na hoja zinazoibuka kuhusu kubanwa kwa uhuru wa vyombo vya habari kwa kusisitiza hakuna uhuru usio na mipaka kwani hata mataifa makubwa ya nje nayo yana mwongozo katika usimamizi wa masuala ya habari.

Amesema habari ni taaluma na kila taaluma inamisingi na miiko ya taalamu yake na baadhi ya wanahabari wanachanganya dhana ya uhuru na miiko ya taaluma, kwa kusema kwanza ujio wa sheria hii ni jambo la kujivunia kwa wanahabari, pia ni mafanikio ya serikali ya awamu ya tano, kwa sababu kwa miaka mingi hakukuwa na sheria ya habari bali kulikuwa na Sheria ya Magazeti.

Aidha, Dk. Abbasi alifafanua kuwa sheria hiyo ya habari imeweka mawanda mapana ya kusimamia ukuaji wa sekta habari kwani imezungumzia haki za wanahabari, uanzishwaji wa taasisi mbalimbali za kusimamia taaluma ya habari, pamoja na kutoa mwongozo wa kuzingatia miiko ya taaluma kama kuzuia utoaji wa taarifa za uongo, kuzuia kuchapisha habari za kashfa, pamoja na kushawishi watu kufanya makosa.

Pia alieleza kuwa hivi karibuni wizara hiyo kwa kushirikiana na TCRA wameidhinisha uanzishwaji wa redio 10 ambazo zitakuwa zikifanya kazi, hivyo hakuna kubanwa kwa uhuru wa habari bali ni usimamizi wa miiko na misingi ya taaluma ndiyo serikali ya awamu ya tano inachokifanya.

Chanzo: habarileo.co.tz