Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Danguro lamvuruga RC Mtwara

Dangururo R C RC (600 X 344) Danguro lamvuruga RC Mtwara

Thu, 16 Feb 2023 Chanzo: Habarileo

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali Ahmed Abbas amelazimika kumuondoa Kamanda wa Polisi Mkoa Mtwara kwenye kikao cha kamati ya Ushauri ya Mkoa na kumwelekeza akasambaratishe dangulo ambalo linatumikisha wanafunzi wa sekondari kwenye biashara ya ngono.

Kanali Abbas ametoa agizo hilo katika kikao hicho kinachoendelea Mkoani hapa baada ya Mwalimu wa Shule ya Sekondari Mkoani hapa kulalamika kuhusu dangulo hilo ambalo linatumika kuzorotesha elimu Mkoani humu.

"Swala la dangulo, RPC nenda sasa hivi kalisambaratishe 'immediately'," amesema huku akionyesha kuhuzunishwa na taarifa hizo. Amesema ni fedheha na ukatili mkubwa kwa watoto wa kike na kiume.

Chanzo: Habarileo