Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Dampo katikati ya makazi lageuka kero Sengerema

Dampo Malalamiko.png Dampo katikati ya makazi lageuka kero Sengerema

Fri, 27 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wakazi wa Mtaa wa Misheni katika Halmashauri ya Wilaya ya Sengerema, mkoani Mwanza, wameitaka Serikali kutatua kero ya dambo lililoanzishwa kwenye makazi yao.

Mmoja wa wakazi wa mtaa huo, Rehema Cosmas ameieleza Mwananchi Digital kuwa kitendo cha kugeuza eneo la makazi yao kuwa dampo, siyo tu kinasababisha harufu mbaya, pia kinahatarisha afya zao na watoto ambao mara nyingi huchezea taka zinazotupwa katika eneo hilo.

"Dampo hili lipo pembeni mwa nyumba yangu; tunapata adha ya harufu mbaya, nzi na wakati mwingine watoto wetu huokota na kuchezea taka zilitupwa dampo, kila wakati tunalazimika kuwadhibiti watoto wasichezee eneo hilo," amesema Rehema.

Malalamiko ya wananchi hao yanaungwa mkono na Mbunge wa Sengerema (CCM), Hamisi Tabasamu ambaye anayetupia lawama uongozi wa halmashauri kwa kushindwa kutatua kero hiyo kwa muda.

Akizungumzia suala hilo, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Sengerema, Binuru Shekidele amesema ofisi yake imeanza kuchukua hatua kutatua kero hiyo.

"Mimi binafsi nitatembelea eneo hilo kushuhudia na kufanya tathmini ya jinsi ya kumaliza kero hiyo ya wananchi," amesema Shekidele

Chanzo: www.tanzaniaweb.live