Mbeya. Madereva wa daladala wa jijini Mbeya leo Jumatatu Machi 18, 2019 wamegoma kutoa huduma ya usafiri kwa shinikizo la kutaka Bajaji zisipite barabara kuu.
Mwananchi imefika kituo cha Uyole na Makasin na kushuhudia umati wa watu waliokwama kutokana na kukosekana usafiri huo.
Hata hivyo, usafiri ambao unatumika kwa sasa ni bodaboda, gari ndogo za kubeba mizigo maarufu ‘kirikuu’, bajaji pamoja na Noah.
Baada mgomo huo Jeshi la polisi kikosi cha usalama barabarani limefika kwenye vituo kutoa msaada kwa wanafunzi kwa kusimamisha mabasi yanayotoka Kyela na Iringa ili kuwasafirisha wanafunzi kwa gharama ya Sh200.
Kwa mujibu wa Issa Kinyunyu dereva wa daladala za Nsalaga/ Stend kuu amesema wataendelea na huduma ya usafirishaji baada ya kukaa kikao na Mkuu wa Mkoa katika viwanja vya Ruanda Nzovwe.
Endelea kufuatilia Mwananchi kujua kinachojiri