Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Daktari asimulia mtoto alivyomeza ndoano

Screenshot 20230716 092555 Chrome Daktari asimulia mtoto alivyomeza ndoano

Sun, 16 Jul 2023 Chanzo: mwananchi.co.tz

Daktari bingwa wa upasuaji wa sikio, pua na koo katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Bugando, Samson Kichiba amesema miongoni mwa matukio ambayo hatosahau ni la mtoto wa mwaka mmoja (jina limehifadhiwa) aliyefikishwa Bugando akipumua kwa shida kutokana na kumeza ndoano iliyokwama katika mfumo wa hewa.

Dk Kichiba ambaye ni Meneja Mkuu wa Kliniki ya Madaktari Bingwa na Bingwa Bobezi ya Bugando iliyoko Nera jijini Mwanza, amesema baada ya kubaini changamoto hiyo walilazimika kutumia zaidi ya saa mbili kufanya upasuaji wa kuondoa ndoano hiyo.

Akizungumza na Mwananchi Digital kuhusu tabia hatarishi kwa malezi ya watoto, Dk Kichiba amesema kukwamwa na ndoano ni miongoni mwa visa vinavyochangia vifo vya watoto kwa kiasi kikubwa hospitalini hapo (bila kutaja idadi), huku akiwataka wazazi kuongeza umakini katika malezi ya watoto katika umri huo.

Sambamba na hilo, amewataka wazazi na watoa huduma ya afya nchini kuwahisha watoto katika hospitali kubwa, ikiwemo za rufaa wanapobaini mtoto amemeza kitu kikakwama sehemu isiyotakiwa (fallen bodies), ili kuwanusuru dhidi ya madhara yanayoweza kujitokeza ikiwemo kifo.

Chanzo: mwananchi.co.tz