Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DSM yatajwa kuwa kinara majanga ya moto nchini

IMG 5199 Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Jumanne Sagini.

Fri, 10 Jun 2022 Chanzo: Tanzania

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Jumanne Sagini, amesema Serikali inafahamu kuwa Jiji la Dar es Salaam linaongoza kwa ajali za moto hivyo wamejipanga kikamilifu kukabiliana na tatizo hilo.

Waziri Sagini ameyasema hayo leo Juni 10, Bungeni jijini Dodoma alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Jimbo la Temeke, Dorothy Kilave aliyehoji kuwa ni lini Serikali itaongeza magari ya zimamoto ili kukabiliana na changamoto ya moto hususan katika masoko ya Jiji la Dar es Salaam.

“Mheshimiwa Spika, ni kweli Serikali inatambua kwamba Dar es Salaam inaoongoza kwa majanga ya moto hivyo kwa kuzingatia hilo, kwenye bajeti ya mwaka huu Serikali inatengeneza magari matatu kwa ajili ya kuongeza nguvu katika Jiji la Dar na maeneo mengine yenye matatizo ya moto,” alisema Waziri Sagini.

Kwa siku za hivi karibuni, Jiji la Dar es Salaam limeandamwa na majanga ya moto hususan katika masoko ya Kariakoo na Karume.

Chanzo: Tanzania