Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DMP awamu ya pili kung'arisha DSM

Zoezi La Kuhamisha Watu Ngorongoro Kukamilika Machi   Mchengerwa.jpeg DMP awamu ya pili kung'arisha DSM

Wed, 21 Feb 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mohamed Mchengerwa amesema Mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam (DMDP) awamu ya pili utajenga barabara za lami katika jiji hilo zenye urefu wa kilomita 250.

Mradi utaanzisha pia mfumo wa udhibiti wa taka ngumu, ujenzi wa masoko 18 pamoja na vituo vya mabasi tisa.

Mchengerwa ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam kwenye hafla ya utiaji saini mkataba wa fedha za mradi huo kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Benki ya Dunia. Waliotia saini ni Waziri wa Fedha na Mpango, Dkt. Mwigulu Nchemba na Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Nathan Belete.

Akizungumza baada ya kusainiwa mikataba hiyo, Waziri Mchengerwa amesema Jiji hilo limekuwa na changamoto ya miundombinu, ikiwamo ya barabara, ambapo awamu ya kwanza ya DMDP iliboresha jumla ya kilometa 207 katika halmashauri tatu zilizokuwa chini ya mradi na zimeleta mabadiliko makubwa.

Kadhalika, amesema kupitia mradi huo master plan ya mifereji mikubwa ya maji ya mvua itaboreshwa na mifereji muhimu itatambuliwa na itajengewa yenye urefu wa kilometa 90.

Naye, Waziri wa Fedha, Mwigulu Nchemba amesema mradi huo utatakelezwa kwa muda wa miaka sita kuanzia mwaka 2024/25 na gharama yake ni EURO milioni 361.1, sawa na shilingi bilioni 988.083.

Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkazi wa Benki ya Dunia, Nathan Belete amesema ni fahari kwao kushiriki katika kukuza na kuendeleza Jiji la Dar es Salaam na kwamba kwa zaidi ya miaka 15, Benki ya Dunia imetoa zaidi ya Dola bilioni 1.5 kwa ajili ya uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live