Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DMO, Mganga mfawidhi waondolewa kwenye vituo vyao

Mndemeeeeeee RC wa Shinyanga Christina Mndeme.

Sat, 27 Jan 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Christina Mndeme amemwagiza Katibu Tawala wa Mkoa Profresa Siza Tumbo kuwaondoa kwenye vituo vya kazi Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Manispaa ya Kahama Dk. Josephati Shani na Mganga Mfawidhi wa hospitali ya Manispaa hiyo Dk. Deo Nyaga kwa kushindwa kusimamia vema majumu yao.

Mndeme ametoa maagizo haya leo wakati akizungumza na watumishi wa sekta ya afya wa Halmashauri za Msalala, Ushetu na Manispaa ya Kahama kama sehemu ya kuwakumbusha wajibu wao wa kufanyakazi kwa kuzingatia kanuni na miongozi ya utumishi wa umma wawapo kazini nasio kuwa na lugha chafu kwa wagonjwa na kutengeneza mazingira ya rushwa. 

Amesema Mgamga Mkuu wa Halmashauri hiyo na mganga mfawidhi wake wameshindwa kusimamia vema majukumu yao hadi kunaibuka kwa kesi mbalimbali ikiwemo ya kusababisha kifo cha mama mjamzito aliyefika kujifungua na kupoteza maisha kwa kukosa huduma, hivyo waletwe wengine wenye uwezo wa kusimamia majukumu haya. 

“Nikuagize Katibu tawala wangu Profesa Siza Tumbo kuwaondoa watumishi hawa mara moja na kuwapeleka kwenye vituo vingine na kuleta wengine ambao wataweza kusimamia majukumu yao, vitendo viovu vinavyofanywa vinatuchafua sisi viongozi na kuifuata halmashauri yetu nasi tutavivumilia viendelee kutokea”Amesema Mndeme. 

Hata hivyo ameongeza kuwa, katika halmashauri ya ushetu kunawatumishi wawili wa kituo cha afya ushetu wamekamatwa na dawa na kuomba wawajibishwe kulingana na mabaraza yao ya kazi na wale watakaobainika baada ya uchunguzi wafutiwe leseni zao na kufikishwa mahakami kujibu tuhuma zinazowakabilia. 

Aidha, amewataka kufanya kazi kwa kuzingatia maadili na miongozi ya kazi zao na kuacha kutengeneza mazingira kwa wagonjwa kwa lengo la kutaka rushwa, kwani wanapobainika na kuondolewa kazi wanasababisha hospitali na vituo vya afya kuwa na uhaba wa watumishi na kuwaumiza wale wanaowategemea majumbani mwao. 

Chanzo: www.tanzaniaweb.live