Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DED wa Itilima afariki dunia ghafla hotelini

Mon, 3 Dec 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Itilima mkoani Simiyu, Mariano Mwanyingu amefariki dunia ghafla usiku wa kuamkia leo Jumamosi Desemba 1, 2018 katika Hoteli ya Peter Palm ya jijini Dodoma.

Taarifa iliyotolewa leo Jumamosi na na Waziri wa Nchi katika Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi) Selemani Jafo imesema marehemu alikuwa jijini Dodoma kuhudhuria kikao cha kikazi.

Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini wa Tamisemi, Rebecca Kwandu akifafanua  zaidi amesema marehemu alikuja juzi Alhamisi jijini Dodoma.

“Alikuja juzi katika kikao cha kazi. Amefariki ghafla katika hotel ya Peter Palm. Alikuwa haumwi," amesema na kwamba taratibu za mazishi hazijafahamika kwa sababu bado watawasiliana na ndugu zake.



Chanzo: mwananchi.co.tz