Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DED akaliwa kooni malipo ya wenyeviti vijiji , vitongoji

Ded Pic DED Buchosa aagizwa kulipa posho wenyeviti wa vijiji, vitongoji

Tue, 9 Nov 2021 Chanzo: mwananchidigital

Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Buchosa llimemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Buchosa mkoa wa Mwanza, Paul Malala kuwalipa malimbikizo ya posho wenyeviti wa vitongoji na vijiji kufikia mwisho wa Novemba.

Kauli hiyo imekuja baada ya Diwani wa Kata ya Kafunzo, Dotto Bulunda kuuliza posho za wenyeviti wa vitongoji na vijiji zitalipwa lini baada ya kulalamikiwa na wenyeviti hao.

Amesema Viongozi hao ndiyo wahamasishaji wakuu wa maendeleo kwenye vijiji hivyo wanatakiwa kuthaminiwa kutokana na mchango wao.

Akijibu hoja hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Buchosa, Paul Malala amesema huwa wanawalipa posho zao kila baada ya miezi mitatu hivyo kufikia mwishoni mwa Novemba watakuwa wamelipwa posho zao.

Amesema Halmashauri ya Buchosa inavitongoji 410 na vijiji 82, hivyo Halmashauri inawajubu wa kulipa posho hizo kwa kuwa wako kwenye bajeti.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Buchosa Idama Kibanzi amesema maagizo ya baraza la Madiwani yanatakiwa kufuata hivyo malipo ya posho zao yasizidi mwenzi huu.

Chanzo: mwananchidigital