Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DED aitaka jamii kulinda miradi ya maji

1d1bc368911e7bfac4f8e204f0179e4a DED aitaka jamii kulinda miradi ya maji

Tue, 21 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bahi mkoani Dodoma, Dk Fatma Mganga amewataka watendaji kuifanya jamii kuwa sehemu ya kuwajibika ili nchi iweze kusonga mbele.

Alisema hayo mwishoni wa wiki wakati wa kutambulishwa kwa mradi wa mapitio ya hatua zilizofikiwa na wadau pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Bahi juu ya uboreshaji wa huduma za maji kutokana na mradi wa kujengea uwezo jamii na asasi za kiraia katika kufuatilia rasilimali za umma (PETS) katika miradi ya maji wilayani humo. Mradi huo unatekelezwa na Mtandao wa Asasi za kiraia Mkoa wa Dodoma (NGONEDO).

Alisema wananchi wanadhani uwajibikaji katika kusimamia miradi ya serikali ikiwemo kulinda miradi ya maji ni kazi ya viongozi na wananchi hawana wajibu.

“Watendaji waifanye jamii kuwa sehemu ya kuwajibika ili nchi isonge mbele, wananchi kazi yao sio kuripoti, tuwajengee uwezo ili wakiona maji yanamwagika watafute ufumbuzi, upotevu wa maji unasababisha kutokuwa na maji ya kutosha,” alisema.

Alisema upatikanaji wa maji hauwezi kufanywa na viongozi peke yao, jamii ushirikishwe ili kubadili mitazamo.

“Tunapokwenda kwenye miradi mipya tuwe makini na pale penye upungufu pajulikane na kufanyiwa kazi, uchumi wa kati uende sambamba na kuchangia shughuli za maendeleo,” alisema.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Kijiji cha Bahi Sokoni, Sifael Mbeti alisema kwenye mradi mpya wa Ngonedo wa kufuatilia matokeo ya utekelezaji wa miradi ya maji iliyopo katika maeneo yao wananchi wanatakiwa kuwa wa kwanza kuwajibika.

“Mimi ni mfuatiliaji sana wa miradi iliyopita, uelewa wa wananchi umeongezeka. Uelewa umeongezeka kijiji cha Bahi Sokoni kina vijiji vinane na vyote vinatoa maji lakini kwenye mapato na matumizi wananchi wanashitikishwa.

“Serikali imetoa fedha za mradi wa maji kijiji cha Bahi Sokoni ambapo mradi huo utapeleka maji Mkakatika, Bahi na Uhelela. Mmoja wa wanakamati wa PETS katika kijiji cha Nguji, Devota Mkoha alisema kabla ya mradi wa Ngonedo kutekelezwa kijijini hapo wananchi hawakuwa na uelewa juu ya kulinda miradi ya maji.

Mratibu wa Ngonedo, Edward Mbogo alisema mradi huo unalenga kufanya mapitio na kufuatilia matokeo ya kufuatilia matokeo ya utekelezaji wa miradi ya maji uliofanyika katika kata nne ili kuona mafanikio.

Pia ufanisi na changamoto zake na hatimaye kuwa na rejeo bora namna bora ya kutekeleza miradi ya kijamii kwa lengo la kuonesha urejesho chanya kwa jamii. Mbogo alisema mradi huo utatekelezwa katika wilaya ya Bahi katika kata nne, Bahi, Mpamantwa, Mundemu na Msisi na vijiji vinne vya Bahi, Mkakatika, Mchito na Nguji.

Mradi huo utatekelezwa kwa muda wa miezi sita kuanzia Julai 2020. Alisema walengwa wa mradi ni asasi za kiraia, jamii. Wajumbe wa kamati za PETS kutoka kata nne na vijiji vinne.

Chanzo: habarileo.co.tz