Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DED: Walimu fichueni walemavu waliofichwa

87c6701a338e94244021f14310cc998b.png DED: Walimu fichueni walemavu waliofichwa

Tue, 8 Dec 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MKURUGENZI Mtendaji wa Halmashauri ya Bahi mkoani Dodoma, Fatuma Mganga amewaagiza walimu kushirikiana na asasi za kiraia ili kufi chua watoto wenye ulemavu waliofi chwa ili wapate haki zao ikiwamo elimu.

Mganga alisema hayo alipofungua mafunzo ya mradi wa elimu jumuishi, yaliyojumuisha walimu wa wilaya hiyo.

Alisema walimu wana wajibu mkubwa katika kushirikiana na asasi ambazo zimekuwa msaada katika kuwaibua watoto wanaokosa haki zao za kimsingi kwa kufichwa majumbani.

“Walimu hakikisheni mnashirikiana na kufanya kazi kwa karibu na asasi za kiraia ambazo ni vinara wa kufichua watoto wenye ulemavu waliofichwa majumbani, kwani kwa kufichwa kunasababisha watoto hao kukosa haki zao za msingi ikiwemo elimu,” alisema Mganga.

Alisema pamoja na kutekeleza mradi wa elimu jumuishi, bado kuna ulazima wa kusaidia ili uweze kuwafikia walengwa hao.

Mganga pia aliwataka walimu waliopewa mafunzo, kutumia fursa ya elimu waliyoipata kufanya kazi kwa vitendo ili wasaidie kupata mbinu zaidi.

Alisema mafunzo wanayoyapata kutoka kwenye miradi mbalimbali inayohusu watoto wenye ulemavu, yatasaidia pia kupata uelewa na mbinu za ufundishaji wanapowafundisha masomo wakiwa darasani.

Mratibu wa mradi huo wilayani Bahi, Jenni Mgidange,alisema bado kuna wazazi na walezi wanaodhani kuwa kumsomesha mtoto mwenye ulemavu ni hasara na ndiyo maana mpaka sasa kuna wazazi wanaowaficha watoto wao majumbani.

Alisema kutokana na imani hiyo iliyojengeka kwa wazazi, walezi na jamii, imewafanya watoto wenye ulemavu ambao wapo majumbani kuendelea kuwa masikini.

Mgidange aliwasihi walimu kuhakikisha wanapowafundisha wanafunzi wenye ulemavu lengo ni kuwafanya wafanye vizuri kitaaluma ili waweze kufikia malengo ya kuondokana na umasikini.

“Walimu ndiyo wa naoweza kuwa dira ya kuwawezesha watoto wenye ulemavu kufanya vizuri kwenye masomo yao kutoka ngazi ya awali hadi vyuo vikuu, lakini hii yote inawezekana pale watakapokuwa karibu nao,” alisema Mgidange.

Dk Wakuru Manini wa Chuo Cha Ualimu Patandi aliwasihi walimu kuwa karibu na watoto wenye ulemavu wakati wote wakiwa ndani na nje ya darasa.

Alisema bado kuna baadhi ya walimu, hawana upendo na ufundishaji wa karibu kwa watoto, hali inaoonesha unyanyapaa na unyanyasaji, unaoweza kuwafanya kukosa haki zao muhimu kama ilivyo kwa wengine.

Chanzo: habarileo.co.tz