Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DED Temeke ataka elimu ya usafi kwa wananchi

Usafi TMK DED Temeke ataka elimu ya usafi kwa wananchi

Sat, 26 Nov 2022 Chanzo: Mwananchi

Mkurugenzi Manispaa ya Temeke, Elihuruma Mabelya sio utaratibu mzuri kuwakamata wananchi kwa kutofanya usafi kabla ya kuwapa elimu kuhusu kazi hiyo.

Ameyasema leo Jumamosi Novemba 26, 2022 alipozungumza na Mwananchi kwa simu, kufuatia hatua ya Ofisi ya Mtendaji wa Kata ya Kizuiani Manispaa ya Temeke kumkamata muuzaji wa magazeti, Sauda Omary.

Amesema shughuli za msingi haziwezi kusimamishwa kwa sababu ya usafi, bada yake watu wapewe elimu kwanza.

“Sio utaratibu ni suala la kutumia tu akili, hatuwezi tukasimamisha shughuli nyingine kama mtu amefanya usafi asubuhi kisha akaendelea na mambo mengine utajuaje.

 “Watu ni lazima wapate habari kila wakati saa 24 na tunajua shughuli za usafi ni lazima zifanyike, huyo anayeuza magazeti kama amefanya usafi saa moja na kuendelea na biasharakuna ubaya gani?” amehoji Mabelya.

Awali akizungumza na Mwananchi Digital baba wa Sauda, Kassim Kibambe amesema mwanaye akiwa kwenye eneo la biashara walifika watu kutoka ofisi ya Kata ya Kizuiani na kuondoka naye.

Amesema kwa kuwa leo ni Jumamosi ya mwisho wa mwezi, hakutakiwa kufanya biashara yoyote hadi itakapofika saa nne.

“Nilipomfuatilia walisema hawezi kutoka bila Sh50, 000 au tusubiri ha Jumatatu apelekwe mahakamani, miliwaambia wamwachie kwa kuwa ni mtoto wa kike nikae mimi hata hivyo walikubali huku wakitaka fedha au kwenda Polisi,” amesema Kibambe.

Ofisa Utumishi wa Manispaa hiyo, Bihaga Yogwa, amekiri kushikiliwa kwa muuzaji huyo wa magazeti, na kueleza kuwa tayari ameshachiwa, akitaka elimu zaidi kutolewa.

“Ni muhimu kuelimishana ule muda wa usafi jamii yote ifanye shughuli hiyo, baada ya hapo kama unataka kuendelea omba kibali kwa Afisa Mtendaji, kwa kuwa biashara ya gazeti inachanganya asubuhi,” amesema Yogwa.

Chanzo: Mwananchi