Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DED Kondoa Mji aahidi kitita watakaofanya vizuri

Dbb8293f05f8186a50db672fd05394fd DED Kondoa Mji aahidi kitita watakaofanya vizuri

Mon, 25 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MKURUGENZI wa Halmashauri ya Mji Kondoa, Msoleni Dakawa ameahidi kutoa Sh 500,000 kwa kila mwanafunzi atakayepata ufaulu wa daraja la kwanza kwa pointi 1 hadi 5 katika mtihani wa utahimilifu mkoa unaotarajia kuanza Februari Mosi 2021.

Alitoa ahadi hiyo wakati akizungumza na wanafunzi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Kondoa .

"Watakaopata daraja la kwanza pointi 1-5 nitampa kila mmoja Sh 500,000 na watakaopata daraja la kwanza pointi 6-9 nitampa kila mmoja Sh 20,000, kwa kuwa najua mkifanya vizuri mtihani huu ni rahisi kufanya vizuri mtihani wa taifa," alisema

Alisema ana imani na wanafunzi watafanya vizuri miaka yote shule hiyo imekuwa ikifanya vizuri na hata kwani hata matokeo ya mwaka jana hakuna mwanafunzi aliyepata daraja sifuri na ni wanafunzi wachache sana walipata daraja la nne.

"Najua siku za kuanza mtihani zimebakia chache ila mkijitahidi kusoma mtafaulu japokuwa wanasema ng'ombe hanenepi siku ya mnada ila anashiba hivyo mkikazana katika siku hizo chache zilizobakia mtashiba kwa kufanya vizuri,"alisisitiza Mkurugenzi huyo.

Aidha alisema itakuwa aibu wanafunzi waliopo Kondoa kushindwa kwenda katika vyuo vikuu vilivyopo Dodoma kama Chuo Kikuu cha Dodoma na Chuo Kikuu cha Mipango lakini pia shule za mkoa wa Dodoma zinapaswa kuwa kinara kwa kuwa ndio makao makuu ya nchi.

Akitoa shukrani Mkuu wa Shule Mwalimu Frola Nussu alisema wamefarijika na ujio wa Mkurugenzi na wakuu wa Idara na wanafunzi walishaahidiwa kupata daraja la kwanza kabla hajaenda hivyo kwa maneno yake watazidisha juhudi na kumuomba Mwenyezi Mungu awapatie afya njema wakati wote wa mitihani.

Kwa upande wao, wanafunzi Getrude Gadau na Tekla Ngalawa wamemshukuru Mkurugenzi kwa kuzungumza nao na kusema kuwa hawakutegemea kama kiongozi kama huyo angewajali hivyo na kumuahidi kufanya vizuri zaidi.

Mkurugenzi amefanya ziara shuleni hapo kwa ajili ya kuwatia moyo wanafunzi wa kidato cha sita 276 wanaotarajia kufanya mtihani wa utahimilifu mkoa kuanzia Februari Mosi ambapo aliongozana na Ofisa Elimu Sekondari na Mkuu wa Idara ya Maendeleo ya Jamii

Chanzo: habarileo.co.tz