Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DED Kaliua asema hawajawahi kukusanya mapato chini ya asilimia 85

Tue, 20 Nov 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Kaliua, Dk John Pima, amesema halmashauri hiyo haijawahi kukusanya mapato ya ndani chini ya asilimia 85 ya malengo yake.

Dk Pima amebainisha hayo leo Jumapili Novemba 18,2018 wakati wa maadhimisho ya miaka mitano tangu kuanzishwa kwa halmashauri hiyo ambapo alisema kwa ujumla imekuwa ikifanya vizuri katika makusanyo ya ndani.

Amesema tangu ianzishwe wamekusanya mapato ya ndani kiwango cha asilimia cha chini kikiwa asilimia 85 na cha juu ni asilimia 130 mwaka wa Fedha uliopita na kuwa ya nne kitaifa katika ukusanyaji wa mapato.

“Kazi kubwa imefanyika katika kipindi hiki tunawashukuru wananchi kwa ushirikiano mkubwa katika kuhakikisha maendeleo yanapatikana, ushirikiano huu, Watendaji  mzidi kuchapa kazi na kuwatumikia wananchi kwa uaminifu na uadilifu mkubwa,” alisema Dk Pima.



Chanzo: mwananchi.co.tz