Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DED Geita kuendelea kusota rumande

Leonidas Felix Leonidas Felix

Fri, 4 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa TAKUKURU mkoa wa Geita, Leonidas Felix (pichani) amesema Mahakama ya Hakimu mkazi mkoa wa Geita imemfutia dhamana aliyekuwa mkurugenzi wa halmashauri ya mji Geita Magret Nakahinga na badala yake ataendelea kusikiliza kesi yake akiwa Gerezani.

Magret Nakahinga ambaye alikuwa mkurugenzi wa halmashauri ya mji Geita katika kipindi cha mwaka 2014 mpaka 2016 anakabiliwa na mashtaka ya kuhujumu mradi wa malisho ya mifugo wa serikali akiwa madarakani.

Aidha Felix anasema katika kipindi cha Julai mpaka septemba 2022 imefuatilia jumla ya miradi 25 yenye thamani ya  zaidi shilingi bilioni 7.

"Baadhi ya miradi kutekelezwa nje ya muda wa mkataba kutokana na mifumo ya malipo kufungwa kabla ya miradi kukamilika kutokana na kuisha kwa mwaka wa Fedha, wizi wa vifaa vya ujenzi kwa baadhi ya miradi, baadhi ya miradi kutekelezwa chini ya kiwango, kwa baadhi ya miradi Fedha kuisha kabla ya miradi kukamilika."

"Mafundi kuchaguliwa wasio nasifa, hivyo kushndwa kutafsiri michoro wakati wa ujenzi jambo ambalo linachelewesha miradi, miradi kuchelewa kuanza kutekelezwa kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo waananchi kusuasua katika kuchangia nguvu kazi kwa kuleta vifaa kama mawe, mchanga, maji hivyo kupelekea miradi kuchelewa," alisema Felix.

Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa imeendelea kuwataka wananchi kutoa taarifa kupitia namba yao ya 113, ili waendelee kuibua na kuwasaka na kuwadhibiti wote wanaojihusisha na vitendo vya Rushwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live