Waziri Ummy amechukua hatua hiyo baada ya kupokea malalamiko ya tuhuma za ubadhirifu wa fedha za miradi ya maendeleo katika Halmashauri hiyo kutoka kwa Wananchi na Viongozi mbalimbali akiwemo Mbunge wa Jimbo hilo Hamisi Tabasamu.
Tuhuma hizo zimeelekezwa kwa Mkurugenzi na baadhi ya Wakuu wa Idara za Halmashauri hiyo na zinaonesha kuwa Mkurugenzi kwa kushirikiana na Wakuu wa Idara hizo wamekuwa wakifanya ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha za Umma zilizotengwa kwa ajili ya shughuli za maendeleo.
Waziri Ummy amemuagiza pia Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI kuunda Timu ya Uchunguzi wa kuchunguza tuhuma hizo haraka.