Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DED Arusha awafunda Wajumbe Baraza la Ardhi

Pima Maji.jpeg Dkt.John Pima akizungumza wakati wa mkutano

Wed, 2 Feb 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Arusha Dkt.John Pima amesema watendaji wa mabaraza ya ardhi ya kata wanatakiwa kutenda haki kwa kuwa wanaiwakilisha Serikali kupitia kwa wananchi wanaowahudumia.

Akizungumza wakati akifungua semina ya siku moja kwa watendaji wa kata,wenyeviti,makatibu,na wajumbe juu ya mabadiko ya sheria ya mabaraza hayo ya ardhi Dkt.Pima,alisema kuwa huo ni mwanzo tu wa kuwawezesha kufanya usuluhishi kwa kuzingatia sheria na kanuni zilizowekwa.

Dkt.Pima alisema kuwa watendaji hao wanaweza kusababisha wananchi wakaichukia serikali au wakaipenda kuona kuwa matokea ya usuluhishi katika mabaraza hayo.

“Nyie ni watu muhimu sana na bado hatuna malalamiko kuhusu mabaraza haya ya ardhi hivyo manake ni kuwa mnafanya kazi vizuri.Sasa endeleeni kufanya usuluhishi kwa kutenda haki ndugu zangu haki ni baraka na mkitenda haki wananchi wataona ni sehemu ya kukimbilia badala ya kukimbia”alisema Dkt.Pima

Aidha alisisitiza kuwa kuna mabadiliko ya sheria ambayo hapo Awali mabaraza yalikuwa yanatoa hukumu badala ya usuluhushi katika maswala ya ardhi ambapo amewataka wajumbe kuhakikisha kuwa wanafanya usuluhushi tu.

Hata hivyo alisema kuwa hatosita kuchukua hatua kwa wajumbe,wenyeviti au makatibu ambao watashindwa kuheshimu mipaka Yao Ili kuepusha migogoro isiyoyalazima.

Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi wa TAMWA,Dkt.Rose Reuben mwanachama wa chama hicho katika mkoa wa Arusha Ashura Mohamed alisema kuwa wameungana na Halmashauri ya Jiji la Arusha kuadhimisha wiki ya sheria Ili kusaidia jamii kupaza sauti na kupinga ukatili wa kijinsia.

Bi.Ashura alisema kuwa uelewa katika Jamii Bado ni mdogo sana hivyo wadau waendelee kutoa elimu kwa wananchi juu ya mambo mbali mbali kama ya miradi,wosia na ukatili ambao kwa Sasa umekithiri.

"Ndani ya Jamii tunazoishi tunashuhudia matukio mengi ya ukatili jambo ambalo sio la kufumbia mambo ukatili havumiliki na tumetoka elimu tukishirikiana na Jiji la Arusha,ambapo tunamshukuru sana dkt Pima kwa kukubali kushirikiana na TAMWA tumegundua wananchi wana uhitaji mkubwa sana"alisema Bi.Ashura Kwa upande wake mwanasheria na wakili bi.Marry Mwita alisema kuwa wiki ya sheria imefanikiwa kwa kiasi kikubwa na walitembelea kata ya Murieti,Moshono na Levolosi na kufikia wananchi zaidi ya 500.

Mbali na kuzungumza na wananchi lakini pia waliweza kuzungumza na wanafunzi katika shule ya sekondari Ngarenaro,shule ya msingi Moshono,Mwangaza na Ngarenaro na kufanikiwa kuzungumza na wanafunzi.

Mada zilizofundishwa ni Migogoro ya Ardhi,Wosia,Miradhi, Mazingira,Mipango Miji,Ukatili wa Kijinsia na Usaidizi wa kisheria.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live