Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC, wadau  wachangia madawati Inzomvu

D27984b52e89867d1dd0d1a25d24d389.jpeg DC, wadau  wachangia madawati Inzomvu

Wed, 14 Apr 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

MKUU wa Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma, Jabiri Shekimweri pamoja na wadau wa elimu wamechangia madawati katika Shule ya Msingi lnzomvu Kata ya Kimagai wilayani humo ili kupunguza idadi ya watoto wanaokaa chini.

Shule hiyo imetajwa kukabiliwa na upungufu wa madawati, matundu ya vyoo, nyumba za walimu hali inayofanya wanafunzi kukaa chini na wengine kujisaidia katika vichaka, jambo ambalo linaweza kuwasababishia kushuka kwa elimu shuleni hapo.

Diwani wa Kata ya Kimagai ambaye ni Mwenyekiti wa maendeleo ya kata, Noha Lento alisema shule hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo upungufu mahitaji ni madawati 344 yaliyopo 211 upungufu ni 133.

Pia matundu ya vyoo yaliyopo ni manane na mahitaji matundu 38, nyumba za walimu mahitaji ni 10 na iliyopo ni nyumba moja na shule hiyo ina jumla ya wanafunzi 1,029.

Kutokana na hali hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Shekimweri na wadau wa elimu wamechangia madawati 50 shuleni hapo.

"Nilikutana na wadau wa elimu hapa wilayani na kuwaomba kwa kushirikiana na ofisi yangu tutengeneze madawati ambayo tulichangia vifaa na kuyatengeneza madawati kwa kupitia karakana ya halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa,”alisema.

Alisema wadau wa elimu hao ni wafanyabiashara wilayani hapo kwa kushirikiana na ofisini yake wametengeneza madawati 200 na wameyagawa kwenye baadhi ya shule zenye uhitaji wa haraka.

Wameanza na Shule ya Msingi Inzomvu ambayo wameipatia madawati 50 angalau waanze kuyatumia.

Kwa upande wa Diwani wa kata hiyo, Noha Lemto wamemshukuru mkuu wa wilaya kwa kuwachangia madawati hayo 50 ambayo yatawasaidia katika kupunguza changamoto ya madawati shuleni hapo

Chanzo: www.habarileo.co.tz