Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC wa Kilosa Tanzania afurahia hati miliki zilizotolewa kwa wananchi

DC wa Kilosa Tanzania afurahia hati miliki zilizotolewa kwa wananchi

Thu, 7 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Morogoro. Kupatikana kwa hati za haki miliki za kimila kwa wananchi wa Wilaya ya Kilosa mkoani Morogoro Tanzania, kumeelezewa kuwa ni mwarobaini wa kupunguza migogoro ya ardhi wilayani humo.

Mkuu wa wilaya hiyo, Adam Mgoi ameyasema hayo leo Jumatatu, Novemba 4, 2019 alipozungumza na waandishi wa habari ofisini kwake.

Amesema kupungua kwa migogoro kumesaidia utekelezaji wa Mradi wa Kuleta Mageuzi katika sekta ya mkaa Tanzania (TTCS) na  Uendelezaji Usimamizi Shirikishi wa Misitu (USM).

Mradi wa TTCS ulianza kutekelezwa 2012 chini ya Shirika la Kuhifadhi Misitu Asili Tanzania (TFCG), Mtangamano wa jamii na usimamizi wa misitu Tanzania (Mjumita), na shirika la kuendeleza Nishati asili Tanzania (TaTEDO) kupitia ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Uswis (SDC).

Mgoi amesema wilaya hiyo kwa muda mrefu ilikuwa na migogoro mikubwa ya ardhi, hivyo Serikali peke yake isingeweza kulimudu suala la kuhakikisha wananchi wote wanapata hati hizo kutokana na kuwapo kwa vijiji vingi wilayani humo.

Amesema baada ya kupatikana na hati wananchi watafaidika katika kupata mikopo ili kujiongezea kipato katika shughuli mbalimbali za kiuchumi wanazozifanya, uwezo wa kutambua eneo la Ardhi kihalali kwamba ni mali yake.

Chanzo: mwananchi.co.tz