Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC mpya Ilala aapishwa

43a38549 8283 483a A404 83d20d45bc7b?fit=640%2C447 DC mpya Ilala aapishwa

Fri, 14 Aug 2020 Chanzo: dar24.com

Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Aboubakar Kunenge amemuapisha Mkuu mpya wa Wilaya ya Ilala Ng’wilabuzu Ndatwa Ludigija alieteuliwa hivi karibuni na Rais Dkt. John Magufuli, ambapo amewataka Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wanasimamia ipasavyo ukusanyaji wa mapato na matumizi ya fedha za serikali.

Aidha amewataka wahakikishe wanaboresha mazingira ya uwekezaji huku akiwataka watumishi wa Mkoa huo kufanya kazi kwa ushirikiano kama timu ili kwa pamoja watatue kero za wananchi.

Rais Magufuli apewa tuzo ya heshimaPia amewahimiza Wakuu wa Wilaya kusimamia ulinzi, usalama na amani hususani kipindi hiki ambacho Taifa linaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Ilala Ludigija ameeleza kuwa ataenda kusimamia ipasavyo utekelezaji wa miradi ya maendeleo pamoja na utatuzi wa kero mbalimbali za wananchi wa Wilaya hiyo.

Mv victoria kuanza kazi jumapiliUganda: Kiongozi wa upinzani akataa kugombea urais 2021

Chanzo: dar24.com