Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC kufikishwa Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma

Onesmo Buswelu Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Onesmo M. Buswelu

Mon, 3 Jun 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Sektretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma, inatarajia kumfikisha mbele ya Baraza la Maadili ya Viongozi wa Umma Mkuu wa Wilaya ya Tanganyika, Onesmo M. Buswelu kwa tuhuma za Ukiukwaji wa Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma

Pia, Sekretarieti hiyo itamfikisha mbele ya Baraza hilo, Yusuph H. Kitumbo, Diwani wa Kata ya Cheyo, Manispaa ya Tabora Mkoani Tabora kutokana na tuhuma hizo

Taarifa ya Sekretarieti imesema Baraza linatarajia kufanya Kikao cha Uchunguzi wa kina Juni 4 na 7, 2024, Saa 3 Asubuhi katika Ofisi za Mkuu wa Mkoa wa Dodoma kuhusu Malalamiko yaliyowasilishwa ambapo Wananchi wanaalikwa kuhudhuria kikao hicho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live