Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC azuia uhamisho walimu bila masurufu

37362 Pic+sabaya DC azuia uhamisho walimu bila masurufu

Thu, 14 May 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

MKUU wa Wilaya ya Hai, mkoani Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya, amezuia uhamisho wa walimu zaidi ya 30 waliokuwa waondolewe katika shule za mjini kwenda shule zenye uhaba mkubwa wa walimu maeneo ya pembezoni, hadi hapo watakapolipwa masurufu yao.

Ole Sabaya aliagiza kusimamishwa kwa zoezi hilo jana, wakati alipokwenda kuzungumza na walimu wa shule za msingi na sekondari za wilaya hiyo, waliokuwa katika mkutano mkuu wa uchaguzi wa viongozi wa Chama cha Walimu (CWT).

“Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Hai (Yohana Sintoo) uko hapa, asihamishwe mwalimu yeyote mpaka muwalipe hawa mnaotaka kuwahamisha kwenda shule za pembezoni.Mheshimiwa Rais Dk. John Magufuli alishaagiza na mimi kazi yangu ni kufuatilia na kusimamia maagizo yake na si vinginevyo,” alisema.

Pia, alimtaka Mwenyekiti wa Chama cha Walimu mkoa wa Kilimanjaro, Omari Mchome, kufikisha salamu zake kwa chama hicho taifa kwamba umefika wakati CWT wanapaswa kufanya mabadiliko ya kimuundo na tathmini ya mali zake zote ili kutafuta njia mpya za kuwasaidia walimu kiuchumi.

“Kawaambie CWT taifa kwamba hili la kuwapa bati 20 walimu wakistaafu ni kuwaumiza kisaikolojia, wabadili gia. Tafuteni namna nyingine ya kuwapa motisha sio hili,”alisema Ole Sabaya.

Kabla ya Ole Sabaya kusitisha mchakato huo, Ofisa Elimu Msingi wa Halmashauri ya Wilaya ya Hai, Christopher Wangwe, aliwatangazia walimu katika mkutano huo kwamba wanatarajia kufanya uhamisho ili kukabiliana na tatizo la uhaba.

Alisema idara ya elimu ya msingi wilayani humo inakabiliwa na changamoto ya ikama, ambapo kuna shule zaidi ya tano zina walimu wanne, huku shule zaidi ya 30 zikiwa na upungufu mkubwa.

“Walimu wanaohamishwa kwenda kufundisha maeneo hayo ambayo mengi ni ya pembezoni, huja na changamoto nyingi za kutaka kubadilishiwa vituo vya kazi huku wakiwa wameshalipwa fedha zaidi ya Sh. milioni tatu,”alisema Wangwe.

“Kwa mfano uhamisho wa walimu wa sekondari 187 waliohamishwa msingi, tayari walimu 56 walishalipwa awamu ya kwanza na sasa wanalipwa awamu ya pili na wataendelea kulipwa kidogo kidogo kadiri fedha zitakavyopatikana.”

Kwa mujibu wa Wangwe, awamu ya kwanza walimu hao walilipwa Sh. 9,080,000 na awamu ya pili watalipwa Sh. 14,191,452.67.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live