Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC azuia ‘kishika uchumba’ mazao ya viungo

5ef8bc7a1bcf25049e27e3a036f9fb66 DC azuia ‘kishika uchumba’ mazao ya viungo

Wed, 25 Nov 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

MKUU wa Wilaya ya Muheza mkoani Tanga, Mwanaasha Tumbo amepiga marufuku vitendo vya wakulima wa mazao ya viungo kuyauza yakiwa bado hayajakomaa kwa kuwa wananyonywa na kuwanufaisha wafanyabiashara.

Alitoa agizo hilo jana wakati wa kikao cha Jukwaa la Mazao ya Viungo lililofanyika katika kata ya Nkumba.

Mwanaasha alisema mkulima atakayebainika anauza mazao hasa ya viungo kabla hayajakomaa atachukuliwa hatua kali za kisheria kwa kuwa atakuwa anahujumu jitihada za serikali za kumkomboa mkulima.

"Kuna tabia imezuka ya kutoa kishika uchumba katika mazao yakiwa shambani naomba niaambie hicho kishika uchumba kinalengo la kumnyonya mkulima mdogo kwani bei ya viungo vikiwa tayari kwa kuuza ni mara ya hicho mnachopewa mazao yakiwa machanga"alisema.

Mwanaasha aliwataka wakulima wazingatie taratibu walizojiwekea kuhakikisha wanauza mazao yaliyokomaa kwa bei elekezi katika vituo ambavyo vipo wilayani humo.

Alimuagiza Mwanasheria wa Halmashauri hiyo aandae Sheria Ndogo ya Kilimo na Uvunaji ili watakaoivunja wachukuliwe hatua.

Ofisa Kilimo, Ushirika na Umwagiliaji Wilaya Muheza Hoyange Marika aliwataka wadau wa kilimo na wakulima wajisajili katika daftari maalumu ili waweze kusaidiwa kwa haraka na serikali changamoto zinazohusu masuala ya kilimo zinapojitokeza.

"Ili kufanya kilimo chenye tija sisi Halimashauri tumeandaa daftari maalum ambalo litakuwa na takwimu halisi za wakulima wa mazao yote hivyo itasaidia kushauriana na kutoa maelekezo kwa walengwa kwa wakati mwafaka"alisema Marika.

Chanzo: habarileo.co.tz