Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC awataka wananchi kuchukua tahadhari ya moto

4381adfa7eb0665490257cc1f6703d9d DC awataka wananchi kuchukua tahadhari ya moto

Thu, 21 Jan 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

MKUU wa Wilaya ya Geita, Fadhili Juma ametoa wito kwa wananchi kuzingatia matumizi sahihi ya nishati ya mafuta, gesi, maji na umeme ili kuepuka matukio ya moto.

Aidha, amezitaka mamlaka zinazohusika na nishati hizo kupunguza gharama za huduma ili wananch wengi waweze kuzitumia.

Fadhili alitoa wito huo juzi wakati wa semina kwa waendesha bodaboda mkoani Geita iliyoandaliwa na Baraza la Ushauri wa Huduma kwa Watumiaji wa Nishati na Maji (Ewura CCC).

Alisema endapo jamii pana itatumia nishati na maji kwa kuzingatia maelekezo ya mamlaka husika ikiwamo Ewura-CCC itasaidia siyo tu kuepusha ajali, bali pia kupunguza gharama za ankara za mwisho wa mwezi hivyo kutumia gharama ndogo na kupata huduma kwa muda mrefu.

"Petroli na gesi zikilipuka hazina urafiki na mtu, tuchukue tahadhari, tuongeze umakini pia majumbani mwetu tunapotumia umeme siyo kitu cha kuchezea, pia maeneo ya kuoshea magari tuwe na umakini, tufuate maelekezo ya Ewura-CCC na Ewura kwa sababu vyombo vingi vya moto ikiwamo bodaboda vinakufa kwa uzembe," alisema.

Ofisa Utawala na Rasilimali Watu kutoka Ewura-CCC, Mwanahawa Said aliwataka wananchi kutambua taasisi hiyo ni kiungo kati ya watoa huduma na wateja na ipo kwa ajili ya kuelimisha matumizi sahihi ya nishati, kuwaunganisha na mtoa huduma pamoja na kuwaelekeza sehemu sahihi ya kupeleka malalamiko yao ikiwamo madai ya fidia.

Mjumbe wa Kamati ya Ewura-CCC mkoa wa Geita, Dotto Paul alisema wametoa elimu ya matumizi sahihi ya nishati na maji kwa waendesha bodaboda ili iwasaidie wao wenyewe kuepuka ajali za mlipuko na kusimama kama mabalozi wa kutoa elimu hiyo kwa wengine kwani hukutana na watu wengi katika mizunguko yao.

Ofisa Utawala Msaidizi wa Ewura-CCC mkoa wa Geita, Wadi Omari alisema wametoa elimu ya matumizi sahihi ya nishati kwa waendesha bodaboda 70 na hadi mwisho wa mwaka huu wanatarajia kuwafikia takribani watu 3,200 mkoa mzima.

Mwenyekiti wa waendesha bodaboda wilaya ya Geita, Daniel Dotto aliishukuru Ewura-CCC kwa elimu hiyo aliyosema imewasaidia kujua wapi kwa kupeleka malalamiko yao na kuomba elimu hiyo kufikishwa mpaka vijijini.

Chanzo: habarileo.co.tz