Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC aviachia vyombo vya dola madai ya dereva wake kumpa rushwa

Sat, 23 Mar 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Hai. Mkuu wa Wilaya ya Hai, Lengai ole Sabaya amepewa dereva mwingine baada ya kumkabidhi katika vyombo vya dola yule wa awali kwa ajili ya uchunguzi huku akisema hata ukikamilika, hamhitaji tena.

“Mimi muda huu nipo vijijini kushughulikia kero za wananchi, tayari nimepewa dereva mwingine na huyo hata kama akiachiwa simhitaji tena.”

Sabaya anamtuhumu dereva wake huyo kutaka kumpa Sh1 milioni anazodai kwamba alipewa na ofisa wa kiwanda kimoja (jina linahifadhiwa) wilayani humo ili ampelekee mkuu huyo wa wilaya ofisini.

Dereva na ofisa huyo walikamatwa Jumatano iliyopita na kuwekwa mahabusu Kituo cha Polisi Bomang’ombe.

Akizungumza na Mwananchi jana, Sabaya alisema suala hilo lipo Takukuru na polisi hivyo, ana imani watafanya uchunguzi wa kina ili kujua chanzo chake.

Ofisa mmoja wa Takukuru ambaye aliomba kuhifadhiwa jina aliiambia Mwananchi jana kwamba suala hilo lipo katika uchunguzi na ukikamilika keshokutwa watatoa taarifa.



Chanzo: mwananchi.co.tz