Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC atahadharisha utegemezi wa faini kama chanzo cha mapato

FEDHA WEB DC atahadharisha utegemezi wa faini kama chanzo cha mapato

Sat, 8 Apr 2023 Chanzo: Mwananchi

Jumuiya ya Hifadhi ya Isawima iliyopo wilayani Kaliua imetakiwa kubuni vyanzo vyake vya mapato badala ya kutegemea faini zitokanazo na mifugo kuingia hifadhini humo kama chanzo chake kikuu.

Akizungumza na wakazi wa kijiji cha Kazanaupate Kata ya Igagala leo Aprili 8, 2023 Mkuu wa Wilaya ya Kaliua Dk Rashid Chuachua ameitahadharisha jumuiya hiyo kuwa muda wa kutegemea faini kama chanzo cha mapato unakaribia mwisho kwakuwa mipango iliyopo ni kuzuia kabisa wavamizi kwenye hifadhi.

“Anzeni kubuni vyanzo vipya vya mapato na kuanza kuondokana na kutegemea faini mnazowatoza wavamizi,”amesema

Akikabidhi mabati, mabomba ya maji machafu na masinki 16 kwa ajili ya ujenzi wa choo cha shule ya msingi Kazanaupate pamoja na Sh1 milioni kijijini hapo, Katibu wa Jumuiya ya Isawima, Hamis Katabanya amesema lengo la kutoa vifaa hivyo ni kuwezesha ujenzi wa choo hicho kilichotitia ili kuhakikisha usalama wa wanafunzi wa shule hiyo.

Amesema jumuiya hiyo imetoa zaidi ya Sh203 milioni kwa kipindi cha miaka mitatu iliyopita katika vijiji vilivyoiunda ili kusaidia miradi mbalimbali ya maendeleo.

Mwenyekiti wa kijiji cha Kazanaupate, Muhsin Omary amesema walitoa sehemu ya eneo la kijiji chao ili kushiriki kwenye uhifadhi wa mazingira kwa manufaa yao na Taifa.

Jumuiya hiyo imeundwa na vijiji 11 vilivyotoa sehemu ya maeneo ya vijiji vyao kwa lengo la kutunza mazingira, kuhifadhi rasilimali zilizopo na kunufaika nazo.

Chanzo: Mwananchi