Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC apiga marufuku wazee kutoka kimapenzi na vijana wadogo

Dc Mgomii (14).jpeg DC apiga marufuku wazee kutoka kimapenzi na vijana wadogo

Fri, 13 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa wilaya ya Ileje nchini Tanzania, Farida Mgomi ametoa wito kwa kina mama wakubwa kuacha tabia na hulka za kutoka kimapenzi na wavulana wadogo kuimri kuwaliko.

Mkuu huyo ambaye alikuwa anaongea katika kijiji kimoja nchini humo alitoa maagizo kwa wanawake kuacha kuwa na uhusiano wa mapenzi na vijana wadogo chini ya umri wa miaka 20, akisema kwamba kufanya hivyo kunamalia nguvu kazi ya taifa ambayo ni vijana.

Bi Mgomi alisisitiza hayo huku akitaja hulka hiyo ambaye imekuwa ikichukua mkondo haswa kwa vijana na kina mama wengi wa maeneo ya mijini kuwa ni kinyume na destruri mila za Kiafrika.

“Vijana tujitahidi sana kufanya kazi, nina taarifa kina mama wenzangu, mimi ni mama mwenzenu lazima niwaambie. Kuna jambo mnanisikitisha sana, kuna kina mama watu wazima wana miaka 40, 50 wanachukua vijana wadogo wenye miaka 20,25,30 wanawaweka kinyumba, wanawaoa watoto wao waliowazaa. Jamani kwani kina mama sisi ndio tuko hivyo? Sisi si ndio walezi?” aliuliza mkuu huyo wa wilaya.

“Mama una miaka 40 unamchukua mtoto wa miaka 18 eti unamlea? Vijana twendeni tukafanye kazi, acheni kufanya mapenzi na kina mama zenu, hao ni wazazi wenu waliowazaa. Una miaka 20 unakwenda kufanya mapenzi na mama wa miaka 50 huyo ni mamako, achene!” alifoka Bi Mgomi.

Mkuu huyo wa wilaya alitema moto akisema kwamba iwe mwisho kwa taarifa kama hizo kutokea kwenye wilaya yake, akisema kwamba hatokubali vitendo hivyo kutokea.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live