Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

DC apiga marufuku watoto kwenda mnadani

KAYANDA Mkuu wa Wilaya ya Karatu, Mh.Abbas Kayanda

Fri, 6 Aug 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mkuu wa Wilaya ya Karatu Mh.Abbas Kayanda, amewataka wazazi kuacha tabia ya kuwapeleka watoto mnadani siku ambazo watoto hao wanatakiwa kufika shule.

Kayanda ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa madarasa na vyoo katika shule ya msingi Bonde la Faru, huku akiwaambia wazazi hao kuwa serikali imedhamiria kujenga miundombinu mizuri itakayo boresha mazingira ya kufundishia na kujifunza.

Aidha amewataka watendaji w aelimu na viongozi wa halmashauri za vijijini kusimamia suala la utoro wa wanafunzi hasa siku za mnada, ili kupata matokeo bora ya ufaulu yatakayo inua wilaya hiyo katika nafasi kitaifa.

Amewataka wazazi kujitahidi kuwapa maarifa ya kutosha wanafunzi hao ili kuinua viwango vya ufaulu vitakavyo wasaidia katika maisha yao baadae.

Amehitimisha kwa kuwasihi wanafunzi kuzingatia masomo kwa bidii kwani elimu ni chachu ya maendeleo kwa jamii.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live